Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ni miongoni mwa vinara wa upachikaji wa mabao kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika akiwa amefunga mabao matano.
Mabao yake mawili kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura yamemfanya mkali huyo wa kuzifumania nyavu afikishe mabao matano na kuwa katika orodha hiyo nyuma ya Moataz Al Mehdi wa Al Nasri ya Libya aliyefunga mabao saba
Kagere ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao mawili katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Katika orodha hiyo pia wamo kiungo Clatous Chama aliyefunga mabao manne, John Bocco mabao matatu na Emmanuel Okwi mwenye mabao mawili.
Takwimu hizi za wachezaji wa Simba zimewatia kiwewe vigogo wa soka Barani Afrika baadhi ya timu zikianza kuhofia kukutana na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara