Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wametumia dakika 270 Uwanjani kucheza michezo ya kiushindani kwa nyakati tofauti na sehemu tofauti.
Simba wameweka rekodi hiyo kutokana na kushiriki michuano miwili tofauti ambayo ni kombe la Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dakika hizo 270 Simba walianza kutumia hivi:
Siku ya Ijumaa dakika 90 walicheza dhidi ya Malindi hatua ya nusu fainali kwenye kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan wakashinda kwa penalti 3-1.
Pia Jumamosi walitumia dakika 90 Uwanja wa Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria walishinda mabao 3-0.
Jana Jumapili walitumia dakika 90 mchezo wa fainali ya Mapinduzi Uwanja wa Gombani Pemba walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Azam FC na kufanya waweke rekodi ya kucheza siku tatu sawa na dakika 270 kwenye mashindano na kutumia viwanja vitatu tofauti.
cc : SalehJembe