Kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla ametakiwa na klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu ya nchini Sweden
Ndemla aliwahi kufanya majaribio katika klabu hiyo mwishoni mwa mwaka 2017
Klabu hiyo imemtaka tena kiungo huyo na anatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini humo kufanya majaribio mengine
Ndemla hajawa na msimu mzuri katika kikosi cha Simba kutokana na uwepo wa ushindani mkali wa namba akiwa amecheza michezo michache ya kikosi cha kwanza
Uongozi wa Simba uko tayari kumuuza kama majaribio yake yatafanikiwa
ADVERTISE HERE