Baada ya kuwaburuza JS Saoura hapo jana, Simba leo inashuka tena katika dimba la Mao kisiwani Pemba kuikabili Azam Fc kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali ambapo Simba imekiongezea nguvu kikosi chake kwa kuwasafirisha Shiza Kichuya, Haruna Niyonzima na Rashid Juma kutoka kikosi cha Dar kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo
Simba ndio timu pekee ambayo imeshinda michezo yote kuanzia hatua ya makundi katika michuano hiyo, ushindi katika mchezo wa leo utaifanya timu hiyo imalize mashindano kwa kuweka rekodi ya aina yake
Mchezo huo utakuwa wa kisasi kwa Simba kwani timu hizo zilikutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Kagame na Azam kushinda mabao 2-1
ADVERTISE HERE