Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wamejikita kileleni mwa msimamo wa kundi D michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jana
Simba ina alama tatu na mabao matatu huku Al Ahly iliyoilaza AS Vita mabao 2-0 ikifuatia nafasi ya pili
AS Vital na JS Saoura zinashika nafasi ya tatu na nne baada kupoteza michezo yao ya mzunguuko wa kwanza
Michezo ya raundi ya pili itapigwa wiki ijayo ambapo Simba itakuwa ugenini nchini Congo kuikabili AS Vita wakati Saoura watasafiri kwenda nchini Misri kuwakabili Al Ahly
ADVERTISE HERE