Mshambuliaji hatari wa Simba Emmanuel Okwi leo amechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Simba dhidi ya JS Saoura.
Okwi ndiye aliyeanza kuifungia Simba bao la kuongoza mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kutengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Kagere katika kipindi cha pili
Okwi alikuwa 'mwiba' mkali kwa safu ya ulinzi ya Saoura ambayo mara kwa mara ilijikuta ikipoteana na kushindwa kumkaba kutokana na ujanja wake wa kuwatoroka walinzi wa timu hiyo na kuvunja mitego ya kuotea.

Hakuna shaka uzoefu wake katika michuano ya Kimataifa utainufaisha sana Simba kwenye michuano hii ya ligi ya mabingwa
Ukiachana na mabao mawili aliyofunga Kagere, Okwi ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo
ADVERTISE HERE