Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo Jumamosi saa 10:00 jioni wanashuka katika uwanja wa Taifa kuikabili JS Sauora kwenye mchezo wa kwanza wa kundi D ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Simba ambayo mwaka huu imerejea kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika baada ya kukosa kwa miaka 15.
Simba iliyozindua kampeni ya YES WE CAN mwanzoni mwa wiki hii, itakuwa inasaka ushindi muhimu ili kuhakikisha inaanza vyema kampeni yake ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Mchezo huo unatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa Simba ambao wamekuwa na kawaida ya kujitokeza kwa wingi Simba inapocheza dimba la Taifa hasa katika michezo ya Kimataifa.
Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson ambaye ataongozana na viongozi waandamizi wa Serikali na klabu ya Simba
Kila la kheri, Wekundu wa Msimbazi, Kila la kheri mabingwa wa nchi.
YES WE CAN!!!!