Aussems awaita mashabiki uwanja wa Taifa kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Jan 2019
Aussems awaita mashabiki uwanja wa Taifa kesho

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewataka mashabiki wa mabingwa hao wa Tanzania Bara kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Yaifa kuwaunga mkono wachezaji wa timu hiyo watakapokuwa wanasaka alama tatu muhimu dhidi ya JS Sauora katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi, kundi D.

Aussems amesema amewaandaa wachezaji wake kushinda mchezo huo wa kesho. Anaamini uwepo wa mashabiki wengi uwanjani utaongeza chachu ya ushindi kwa kikosi chake

"Mipango yetu kuwapa raha mashabiki, mechi hizi ni ngumu na lazima tujifue vyema kuhakikisha tunashinda

"Tutakuwa nyumbani ni muhimu kupata matokeo mazuri kabla ya kwenda kucheza ugenini.

"Mashabiki wetu wasiwe na hofu kabisa na waje uwanjani kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji kwani, uwepo wao ni muhimu sana kwetu," amesema Aussems

Simba imekuwa ikijifua katika uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo huo wa ufunguzi wa hatua ya makundi msimu huu

Licha ya kumkosa kiraka Erasto Nyoni, Kocha Aussems atamtumia Mganda Juuko Murshid sambamba na Paschal Wawa katika safu ya ulinzi.

Tangu juzi Aussems amekuwa akiwatumia wachezaji hao pamoja katika mazoezi ya mabingwa hao wa kihistoria Afrika Mashariki.

JS Sauora imewasili nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo huo ambao hakuna shaka utakuwa mgumu sana kwa upande wao kutokana na uimara wa kikosi cha Simba hasa kinapocheza kwenye dimba la Taifa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’