Wapinzani wa Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa, JS Saoura wanatarajiwa kuwasili leo Alhamisi usiku kwa ndege ya kukodi wakitokea nchini Algeria.
Kikosi cha JS Sauora kinatua nchini kikiongozwa na Mtanzania Thomas Ulimwengu aliyesajiliwa na klabu hiyo hivi karibuni baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Hillal.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa JS Sauora kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, hatua ya makundi.
Wenyeji wa mchezo huo Simba wameendelea kujifua katika uwanja wa Boko Veterans kujiandaa kuwakabili Wa Algeria hao katika dimba la Taifa keshokutwa Jumamosi, Januari 12 2019
ADVERTISE HERE