Kikosi cha Simba kilichobaki visiwani Zanzibar kesho Ijumaa kitashuka katika dimba la Amaan kuikabili Malindi Fc kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi.
Simba imemaliza kileleni mwa kundi A baada ya kushinda michezo yake yote na sasa itachuana na Malindi iliyomaliza katika nafasi ya pili kundi B.
Mchezo huo utapigwa saa mbili na robo usiku. Mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya Azam Fc dhidi ya KMKM utapigwa saa kumi na robo jioni.
Kikosi kilichobaki Zanzibar kimeongezewa nguvu na wachezaji wa kikosi cha vijana, Simba B.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza tayari wako jijini Dar es salaam wakiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Sauora utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye dimba la Taifa.
ADVERTISE HERE