Pluijm anaamini Simba itafanya maajabu ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jan 2019
Pluijm anaamini Simba itafanya maajabu ligi ya mabingwa

Kocha Mkuu wa Azam Fc Hans van Pluijm ameitabiria Simba kuwa itafika mbali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Jumamosi ikianza kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya JS Sauora ya Algeria.

Pluijm ambaye kikosi chake kimetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi kama ilivyo kwa Simba, amesema mabingwa hao wa Tanzania Bara wana kikosi imara kinachoweza kufanya mambo makubwa msimu huu.

"Simba ina kikosi imara sana. Ina wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa, wachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa Afrika, nadhani wanaweza kufika mbali katika michuano ya ligi ya mabingwa," amesema Pluijm

"Wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanatumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kushinda michezo yao yote. Wahakikishe wanafunga mabao mengi nyumbani"

Simba imepangwa kundi D pamoja na Al Ahly, AS Vita na JS Sauora.

Januari 12 itacheza nyumbani dhidi ya JS Sauora, Jan 19 itasafiri kwenda DR Congo kuikabili AS Vita kisha kuelekea nchini Misri kuikabili Al Ahly mwanzoni mwa mwezi wa pili

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
18m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’