Wakati kikosi cha kwanza cha Simba kikirejea jijini Dar es salaam leo kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Sauora utakaopigwa Jumamosi Jan 12, baadhi ya wachezaji watabaki visiwani Zanzibar na wataungana na wachezaji wa kikosi cha vijana cha mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Simba itaendelea kubaki visiwani Zanzibar baada ya kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi itakayofikia tamati Januari 13.
Wachezaji wanaobaki visiwani Zanzibar:
Ally Salim
Zana Coulibaly
Asante Kwasi
Paul Bukaba
Adam Salamba
Yusuph Mlipili
Mo Ibrahim
Abdul Suleiman
Wachezaji hao wataungana na baadhi ya wachezaji wa Simba B kumalizia hatua iliyobaki ya michuano ya kombe la Mapinduzi.
ADVERTISE HERE