Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinatarajiwa kuwasili leo Jumatano kutoka visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo kinaondoka visiwani humo kikiicha timu katika hatua ya nusu fainali.
Simba inarejea Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura utakaopigwa Jumamosi, Januari 12 2019
Aidha wachezaji wa kikosi cha timu ya vijana ya Simba wataelekea visiwani Zanzibar kumalizia michezo iliyobaki kwenye michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi.
Wakati Simba ikirejea jijini Dar leo, wapinzani wao JS Saoura watatua kesho kutoka kwao Algeria.
ADVERTISE HERE