Niyonzima nyota wa mchezo dhidi ya Mlandege Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Jan 2019
Niyonzima nyota wa mchezo dhidi ya Mlandege Fc

Kiungo fundi Haruna Niyonzima jana aliisaidia Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege Fc kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi kundi A.

Niyonzima alifunga bao pekee la Simba  kupitia mkwaju wa penati na kuwahakikishia mabingwa hao wa Tanzania Bara ushindi wa tatu mfululizo na kumaliza hatua ya makundi wakiwa wameshinda michezo yote.

Simba imetinga nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa kileleni mwa kundi A baada ya kujikusanyia alama tisa.

Niyonzima alikuwa katika kiwango bora kwenye mchezo huo na haikushangaza kwa yeye kuteuliwa kuwa nyota wa mchezo na kukabidhiwa zawadi ya mpira na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mohamed Ahmada

Bila shaka kocha Patrick Aussems amemuona na huenda akampa nafasi kwenye mchezo ujao wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Sauora,kutegemeana na mahitaji ya timu.

Niyonzima anakabiliwa na ushindani mkali wa namba kutoka kwa viungo wanaon'gara zaidi kwa wakati huu katika kikosi cha Simba Clatous Chama 'CCC' na Hassan Dilunga 'HD'

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’