Uongozi wa klabu ya Simba mapema leo Jumanne, Januari 08 2019 ulizindua kampeni ya 'YES WE CAN' mahsusi kwa ajili ya kuipa sapoti Simba kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Afisa habari wa Simba Haji Manara ambapo mbali na mambo mengine, Manara ametaja viingilio vya mchezo wa Jumamosi dhidi ya JS Sauora.
Kutakuwa na viingilio vya aina tatu ambavyo ni Platinum, VIP B na Mzunguuko.
VIP B ni Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/- na tiketi za Platinum ni Tsh 100,000/-
Manara amesema tiketi ya Platinum itakupa fursa ya kuchukuliwa katika hotel ya nyota tano ya Serena,kwa kupelekwa uwanja wa Taifa katik gari yenye hadhi (luxury bus) huku ukisindikizwa na king’ori cha Polisi, hiyo ni kwenda na kurudi toka Serena hotel na uwanja wa Taifa.
Ndani ya uwanja wa Taifa wenye tiketi za Platinum wataendelea kupata huduma mbalimbali kwa ajili yao ikiwa ni pamoja na kupewa jezi za Simba bure