Kikosi cha kwanza cha Simba kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Sauora utakaopigwa Jumamosi, Januari 12 2019
Aidha, wachezaji wa kikosi cha vijana Simba B wanatarajiwa kuongezwa visiwani Zanzibar kumaliza michezo iliyobaki ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Leo Simba itashuka dimba la Amaani kuikabili Mlandege Fc kwenye mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi Simba ikiwa imejihakikishia kutinga nusu fainali baada ya kushinda michezo yake miwili ya kwanza
Kikosi cha kwanza cha Simba huenda kikaondoka kesho visiwani Zanzibar kurejea jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE