Simba yataka utulivu majeraha ya Nyoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jan 2019
Simba yataka utulivu majeraha ya Nyoni

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara umesema kuwa taarifa rasmi kuhusu kiraka Erasto Nyoni aliyeumia jana visiwani Zanzibar wakati akiitumikia Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, zitatolewa kesho

Manara amesema taarifa zilizosambaa leo kuwa Nyoni atakuwa nje kwa wiki tatu si rasmi kwa kuwa hazikutolewa na uongozi wa Simba.

Manara amesema taarifa sahihi zitatolewa kesho kwenye Mkutano na Waandishi wa habari ambao awali ulikuwa ufanyike leo lakini umeahirishwa.

"Kuna taarifa za upotoshwaji zinazoendelea kusambazwa mitandaoni juu ya majeraha aliyoyapata beki wetu Erasto Nyoni kwenye mchezo wa dhidi ya KMKM uliochezwa jana.

"Nyoni anaendelea na vipimo zaidi leo hapa Dar es Salaam na taarifa ya ukubwa wa jeraha lake na aina ya tiba atakayopata itatolewa na Msemaji wa Klabu katika mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika kesho Jumanne saa 7:00 mchana," imesema taarifa ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’