Simba kuanza na Chipukizi Fc kombe la Mapinduzi leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jan 2019
Simba kuanza na Chipukizi Fc kombe la Mapinduzi leo

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanaanza kampeni ya kuwania taji la kombe la Mapinduzi kwa kuchuana na Chipukizi Fc katika mchezo unaotarajiwa kupigwa saa mbili na robo usiku.

Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Patrick Aussems leo huenda akashusha kikosi chake kamili kwani Simba itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura utakaopigwa Jumamosi ya Januari 12, 2019

Mtaribu wa Simba Abbas Ally amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri

"Tumekuja visiwani Zanzibar tukiwa na kikosi chetu kamili kwani tunatambua umuhimu wa michuano hii," amesema Abbas

"Tumejiandaa vizuri na wachezaji wetu wako tayari kwa ajili ya mchezo huo"

Kikosi cha Simba kitakuwa Zanzibar hadi Januari 08 ambapo kama timu hiyo itafuzu hatua inayofuata wachezaji wa kikosi cha pili wataendelea kubaki visiwani humo wakati wale wa kikosi cha kwanza watarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya JS Souara.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’