Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetaja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya JS Saoura utakaochezwa Januari 13 jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi Joshua Bondo kutoka Botswana atasimama katikati kupuliza kipyenga cha pambano hilo ambapo atasaidiwa na wenzake Oamogetse Godisamang na Godfrey Moemedi Monakwane ambao pia wanatokea nchini Botswana kama mwamuzi msaidizi namba moja na namba mbili.
Leso Kutlwano kutoka Botswana yeye atakuwa mwamuzi wa mezani katika pambano hilo huku James Leonard Mwenda kutoka Malawi akipewa jukumu la kuwa Kamishna wa mchezo.
Alexander Sakyi Asante kutoka Ghana yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa mchezo huo wakati Mganda Dixon Adol Okello yeye atakuwa Ofisa wa Ulinzi.