Mtendaji Mkuu wa Simba (CEO) Cresentius Magori amesema taarifa za Mshambuliaji wa Nkana FC Walter Bwalya kutakiwa na klabu hiyo kwa wakati huu sio za kweli kwani hata kanuni za kumsajili haziruhusu maana ameshachezea timu iliyoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa.
Aidha, kuhusu Okwi kutakiwa na Kaizer Chiefs Magori amekiri taarifa hizo ni za kweli.
"Ni kweli walituambia kwa mazungumzo ya mdomo lakini hadi sasa hakuna ofa yeyote iliyotufikia kutoka huko na kama wataleta basi Bodi ya Wakurugenzi itaamua kama aondoke au la.
"Pia kocha atatoa mamauzi kama aondoke au la na akiondoka mbadala wake ni nani atakayeziba pengo hilo maana tuna michuano mikubwa ya klabu bingwa Africa inatukabili , Okwii ni mchezaji mhimu ndani ya simba na kaifanyia makubwa mengi hakuna mtanzania asiyelijua hilo," amesema.
Katika hatua nyingine, Magori ameomba radhi baada ya timu hiyo kutolewa mapema kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC).
"Niwaombee radhii wanasimba kwa kutolewa mapema katika michuano ya FA kila mwanasimba ameumizwa na hili hivyo tunapambana kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu ligi baado mbichi hii"
"Leo tunakaa na mwalimu kuzungumzia kuhusu benchi la ufundi kuna baadhi ya wachezaji amewaona ndani ya Tanzania na njee Tanzania kama atahitaji kuboresha kikosi chake kabla ya michuano hii kuanza ni uamuzi wake kama ataona hakuna haja sisi tunamsikiliza yeye na ripoti yake tutaiwasilisha bodi ya wakurugenzi Jumamosi."