Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo imeanza rasmi jana.
Simba imekwenda Zanzibar ikiwa na kikosi chake kamili kilichosheheni nyota wake wote.
Benchi la Ufundi la Simba linaloongozwa na kocha Patrick Aussems limepanga kutumia michuano hiyo kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura utakaopigwa Jumamosi, Januari 12 katika dimba la Taifa.
Kama Simba itafanikiwa kufuzu raundi inayofuata baadhi ya wachezaji wataendelea kubaki visiwani Zanzibar huku kikosi cha kwanza kikitarajiwa kurejea jijini Dar es salaam Januari 08, 2019 tayari kwa mchezo dhidi ya JS Souara
Simba itashuka dimbani keshokutwa Janurari 04, kucheza na Chipukizi.
ADVERTISE HERE