Simba iko tayari kuchuana na vigogo Afrika - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jan 2019
Simba iko tayari kuchuana na vigogo Afrika - Manara

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesisitiza kuwa timu hiyo iko tayari kuchuana na vigogo kuwania ubingwa wa Afrika na wale wasioamini wafike uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi kati ya Simba dhidi ya JS Sauora utakaopigwa Jumamosi, Januari 12 2019.

Manara amesema Simba haihofii majina ya timu ilizopangwa nazo kundi D na watalithibitisha hilo kwa kuchukua alama zote tatu katika michezo yao itakayopigwa kwenye dimba la Taifa.

"Sahau kuhusu kundi letu la Ahly, Vita na Waalgeria,Simba hata ingepangwa na Barcelona, Man city na Juventus kwa hapa Dar tungechukua points zote tisa!!," ameandika Manara katika mtandao wake wa Instagram.

"Kama unadhani Simba ni dhaifu jisogeze Taifa jumamosi ya Januari 12 alasiri ujue tunafananaje," aliongeza Manara

Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya wachambuzi wa soka ambao wamekuwa wakitoa maoni kuwa Simba haitafua dafu kundi D kutokana na kupangwa na timu ambazo zimekuwa na mafanikio zaidi yake.

Lakini uongozi wa Simba na hata kocha Patrick Aussems amesisitiza kuwa kila timu ina nafasi sawa kundi D, kinachohitajika ni maandalizi na kujipanga ili kupata matokeo mazuri katika michezo ya nyumbani.

Simba imeweka mkakati wa kuhakikisha inashinda michezo yake yote itakayochezwa kwenye dimba la Taifa.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’