Wakati leo sikukuu ya mwaka mpya inasherehekewa kote duniani, beki Asante Kwasi anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Kwasi aliyetua Simba msimu uliopita akitokea Lipuli Fc wakati wa usajili wa dirisha dogo, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Msimu huu amekuwa haonekani mara kwa mara dimbani kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara huku piaushindani wa namba kati yake na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' ikiwa sababu nyingine.

Tunamtakia kila la kheri katika siku yake hii muhimu.
ADVERTISE HERE