Simba ianze na alama tatu za JS Saoura

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jan 2019
Simba ianze na alama tatu za JS Saoura

Jumamosi ya Januari 12 2019 Simba itakuwa uwanja wa Taifa kuikaribisha JS Saoura ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika, kundi D.

Simba ina faida ya kucheza nyumbani lakini pia itakuwa inakutana na timu ambayo kimsingi bado ina ugeni katika michuano ya Afrika.

Hii ni mara ya kwanza kwa JS Saoura kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, hatua ya makundi.

Timu hiyo haina miaka mingi sana tangu ianzishwe kwani ilianzishwa mwaka 2008.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Algeria, JS Saoura inashika nafasi ya nne ikiwa imejikusanyia alama 23 baada ya kushuka dimbani mara 15. USM Alger ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 33.

Timu hiyo pia ina wachezaji wawili tu wa kigeni mmoja akiwa ni Mtanzania Thomas Ulimwengu aliyesajiliwa mwezi uliopita baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Hilal ya Sudan

Simba imejiwekea mkakati wa kushinda michezo yake yote ya nyumbani ili kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Matokeo ya ushindi dhidi ya JS Saoura itakuwa ni mwanzo mzuri kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara katika kampeni yao ya kutinga robo fainali.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’