Simba kuendelea na mazoezi leo, tayari kwa safari ya Zanzibar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jan 2019
Simba kuendelea na mazoezi leo, tayari kwa safari ya Zanzibar

Simba kesho inakwenda Zanzibar tayari kuwasha moto katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, huku Kocha Patrick Aussems akiamua kukomaa na wachezaji 13 ambao hawakupewa mapumziko kama wenzao.

Kocha huyo kutoka Ubelgiji aliamua kuwapa nyota wake wa kikosi cha kwanza mapumziko mafupi ya siku tatu, huku akikomaa na wengine walioshindwa kuibeba timu hiyo mbele ya Mashujaa FC kwenye mechi yao ya Kombe la FA.

Wachezaji waliokuwa mapumziko wataungana na wenzao hao 13 leo Jumanne kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kupanda boti kuelekea Zanzibar.

Wachezaji hao 13 waliokuwa wakipigishwa tizi Gym iliyopo hoteli wanayoweka kambi timu hiyo na Kocha wa Viungo, Adel Zrane ili kuwekwa fiti ni pamoja na Deogratius Munishi ‘Dida’, Ally Salim, Zana Oumar Coulibaly, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yusuf Mlipili, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Abdul Selemani, Adam Salamba na Haruna Niyonzima.

Kocha Aussems alisema aliamua kuwapigisha tizi wachezaji hao kama mpango wa kuiandaa timu yake kwa ajili ya mechi ngumu inayowakabili mbele hasa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria itakayochezwa Januari 12 kwenye Uwanja wa Taifa.

"Wanaendelea kufanya mazoezi ni kama sehemu ya maandalizi ili kuwa sawa katika hali ya kushindana kama wale ambao niliwatumia ili yoyote atakayepata nafasi katika hizi mechi ngumu za Kimataifa afanye kitu atakachotakiwa kufanya."

"Wachezaji wote watakutana kesho (leo Jumanne) na Jumatano tutakwenda Zanzibar kwa michuano ya Mapinduzi, tutayatumia kama sehemu ya maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa. Tutacheza mechi za Januari 4 na 6, lakini ikifika Januari 8 nataka timu iwe Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mechi na JS Saoura." alisema.

Kocha Aussems alisema anajivunia kucheza mechi ya kwanza uwanja wa nyumbani na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kuipa nguvu timu na kuishangilia akiamini kutawasaidia kupata ushindi katika mchezo huo mgumu.

Naye beki Mlipili alisema wanayatumia mazoezi hayo kujiweka fiti kwa mechi za Mapinduzi akiahidi kurejesha heshima yao kwa mashabiki na kula sahani moja na wenzao walio fiti zaidi kikosini.

"Mapinduzi yaweza kuwa michuano kwetu kwa tusiopata nafasi ya kucheza Ligi Kuu kwa kuonesha kiwango chetu na kumshawishi Kocha," alisema Mlipili.

cc : Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
10h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’