Mwekezaji na Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mwenyekiti wa Simba, Bodi ya Wakurugenzi, Afisa mtendaji mkuu (CEO), Sekretariet ya klabu, Benchi la Ufundi, Wachezaji, Wanachama na Mashabiki wote wa Simba, tukiwa tumebakiza saa chache kufunga mwaka huu, kwa dhati kabisa tuwashukuru nyote ambao kwa namna moja au nyingine mmeifanya klabu yetu kuwa bora kwa sana 2018.
Kimsingi Mwaka huu tumefanikiwa katika mambo makubwa matatu;
A) kushinda Ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania
B) Kufuzu hatua za makundi za ligi ya mabingwa barani Afrika
C) Kubadilisha muundo na mfumo wa klabu yetu kuwa wa kisasa zaidi na kutengeneza njia sahihi za kuifanya simba kuja kuwa klabu ya mfano sio tu Tanzania bali Afrika nzima.
Kwa kweli tunapaswa kujipongeza wote na pia kwa pamoja tuendeleze umoja na mshikamano wetu ndani ya klabu hususan ktk mwaka unaokuja,ambapo tunakwenda kushiriki ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mwisho
klabu inawaomba radhi wale ambao kwa namna yoyote ile walikwazika ktk utendaji wa nje ya Uwanja,yote ilikuwa katika kutekeleza majukumu yetu klabuni
Kwaheri 2018
Karibu 2019