Bocco awapigia hesabu Waarabu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Dec 2018
Bocco awapigia hesabu Waarabu

Nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi licha ya kupangwa na timu mbili kutoka mataifa ya Uarabuni katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wamejipanga kuweka rekodi kuhakikisha wanawafunga kila watakapokutana nao na kusonga mbele katika hatua hiyo.

Bocco ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosaidia kikosi hicho kutinga hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa katika Kundi D.

Kundi hilo lina timu za Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria pamoja na AS Vita ya DR Congo huku mechi yao ya kwanza ya hatua hiyo wakitarajia kucheza Januari 11 mwakani.

Bocco amenukuliwa na gazeti la Championi akisema kuwa wameona kundi ambalo wamepangwa na tayari wameanza kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanazifunga timu zote ambazo watacheza nazo katika Uwanja wa Taifa zikiwemo Al Ahly na JS Saoura.

"Mashindano haya ni magumu na kundi tayari tumeliona, kwetu hili ni kundi zuri na tutapambana kwa ajili ya kusonga mbele katika kundi kwa kushika nafasi za juu. “Watu wamekuwa wakiona tukipoteza mara nyingi mbele ya timu za Kiarabu lakini kwa msimu huu niwaambie kwamba tutaweka historia kwa kuwachapa wote ambao tutacheza nao.

"Sisi hatuchezi kwa historia eti kwamba tulipoteza mechi na timu fulani bali tunacheza kwa kilichopo mbele yetu, kwa hiyo naamini tutajipanga vizuri kwa msimu huu na lengo letu ni kuweka rekodi" alisema Bocco.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’