Aussems ataka Coulibaly apewe muda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Dec 2018
Aussems ataka Coulibaly apewe muda

Mashabiki wa Simba walikuwa na matumaini makubwa kwa usajili wa beki mpya Zana Coulibaly aliyetua Simba akitokea ASEC Mimosas katika usajili wa dirisha dogo lililofungwa Disemba 15.

Mchezaji huyo ambaye alisajiliwa kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe ambaye alipata majeraha makubwa wakati akiitumikia timu ya Taifa, bado hajaonyesha kama anaweza kuvaa viatu vya Kapombe.

Akiwa ameitumikia Simba kwenye michezo mitatu, bado hajaonyesha makali yake hasa ikizingatiwa wengi wanamlinganisha na Kapombe ambaye kiwango chake kilikuwa juu zaidi. Kimsingi Kapombe ndiye winga/beki bora wa upande wa kulia nchini.

Juzi baada ya mchezo dhidi ya Singida United, Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na subira ili kupata mambo mazuri kutoka kwa Coulibaly ambaye anao uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo mkabaji.

Aussems alisema Coulibaly hakuwa dimbani kwa takribani miezi mitano hivyo anahitaji muda wa kucheza ili aweze kurejesha makali yake.

"Zana hajacheza kwa takribani miezi mitano, anahitaji kucheza mechi nyingi ili aweze kurejesha makali yake. Sina wasiwasi na uwezo wake, ni mchezaji mzuri, " alisema Aussems.

Coulibaly anatarajiwa kuongezwa kwenye kikosi cha Simba kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi. Simba ikitarajiwa kushuka dimba la Taifa Januari 11 2019 kuikabili JS Souara ya Algeria

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’