Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba huenda wakalazimika kupeleka kikosi cha Vijana visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Ratiba ya michuano hiyo inayofanyika kila mwaka inaonyesha Simba itashuka dimbani Januari 04, 2019 kuikabili Chipukizi.
Hata hivyo, Januari 11 Simba inakabiliwa na mchezo muhimu wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi dhidi ya JS Souara ya Algeria
Michuano ya kombe la Mapinduzi itamalizika Januari 12.
Kuna mapendekezo kwa baadhi ya wachezaji ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza wajumuishwe na wengine kutoka timu ya vijana kwenda kushiriki michuano hiyo ili kuwaimarisha.
Mwaka huu michuano ya kombe la Mapinduzi inashirikisha timu kutoka Tanzania pekee baada ya URA kutoka Uganda kujitoa.
Bingwa wa michuano hiyo atashinda kombe na fedha taslim Tsh Mil 15