Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alifurahishwa na kikosi chake jana kilichofanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United.
Aussems amempongeza winga Shiza Kichuya kwa kuisaidia Simba kwenye mchezo huo akifanikiwa kufunga mabao mawili na kutengeneza bao jingine moja
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema timu yake ina wachezaji wengi wazuri, hivyo mchezaji anapopewa nafasi ni vyema akaitumia ili ajitengenezee mazingira mazuri ya kuendelea kucheza.
Aidha Aussems amsifu beki mpya wa timu hiyo Zana Coulibaly kuwa anaendelea kuimarika kikosini Simba. Beki huyo ameongezwa kwenye kikosi cha Simba kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi.
Aussems ametoa mapumziko ya siku tatu kwa wachezaji wake kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya.