FT : Simba 3-0 Singida United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Dec 2018
FT : Simba 3-0 Singida United

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wamerejesha furaha Msimbazi baada ya kuifumua Singida United mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems leo alipanga kikosi cha maangamizi ambacho kwa hakika kimeingamiza Singida United iliyokuwa na wakati mgumu katika mchezo huo.

Shiza Kichuya leo alikuwa nyota waΒ  kikosi cha Simba baada ya kuhusika katika mabao yote yaliyofungwa na washiriki hao wa michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi

Katika dakika ya 17 Kichuya alimtengenezea Bocco aliyefunga bao lake la tatu msimu huu huku Kichuya tena akifunga mabao mengine mawili kwenye kipindi cha pili yote yakitengenezwa na Cletous Chama 'CCC'

Ushindi ni matokeo stahiki kwa Simba iliyochocheza kandanda safi kwa muda wote wa mchezo.

Simba imefikisha alama 33 baada ya ushindi wa leo, imeendelea kusalia katika nafasi ya tatu.

Kama itashinda michezo yake minne ya kiporo, Simba ina uhakika wa kuiengua Azam Fc katika nafasi ya pili.

Leo Azam imepoteza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuchapwa mabao 2-0

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’