Manara awaita mashabiki uwanja wa Taifa, mchezo dhidi ya Singida United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Dec 2018
Manara awaita mashabiki uwanja wa Taifa, mchezo dhidi ya Singida United

Baada ya kuwafahamu wapinzani wao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ligi kuu leo ambapo itacheza dhidi ya Singida United.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Taifa na utaanza saa moja usiku.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Simba.

"Matokeo tunayohitaji katika mchezo huo ni ushindi. Tunawataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwaunga mkono wachezaji wetu watakaotuwakilisha katika mchezo huo," amesema

Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imeshuka dimbani mara 13 na kujikusanyia alama 30.

Kutokana na kuwa na mchezo mingi ya kiporo (minne), Simba inahitaji kushinda michezo hiyo yote ili kuendelea  kuwa sambamba katika mbio za ubingwa na timu za Yanga na Azam Fc ambazo ziko kileleni.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wana matumaini makubwa ya kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Taifa leo

Simba imekuwa na rekodi nzuri ya kupata ushindi dhidi ya Singida United ambapo msimu uliopita kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa taifa Simba ilishinda 4-0 na kisha kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa duru ya pili uliopigwa mkoani Singida.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’