Droo ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi inafanyika leo nchini Misri kuanzia saa moja jioni kwa saa za Tanzania.
Simba imewekwa chungu namba tatu sambamba na Asec Mimosas, CS Constantine na Orlando Pirates na kwa kuwa timu zilizokwenye kapu moja hazipangwi kundi moja, Simba imezikwepa timu hizo.
Miongoni mwa timu ambazo zinaweza kupangwa kundi moja na Simba ni pamoja na Al Ahly (Misri), Eperance (Tunisia), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) na Wydad AC (Morocco) zilizo chungu cha kwanza, AS Vita Club (DRC), Club Africain (Tunisia), Horoya AC (Guinea) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini). Chungu cha nne kina timu za FC Platinum (Zimbabwe), Ismaily (Misri),JS Saoura (Algeria) na Lobi Stars (Nigeria)
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' ndiye mwakilishi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara katika droo hiyo inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania.