Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba keshokutwa Jumamosi, Disemba 29 2018 wanashuka katika dimba la Taifa kuikabili Singida United katika mchezo wa ligi kuu raundi ya 18.
Hakuna shaka katika mchezo huo wa kufunga mwaka 2018 Simba itashusha 'mziki kamili' hasa baada ya hapo jana 'kujeruhiwa' na Mashujaa Fc katika mchezo wa kombe la FA (ASFC).
Baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la FA, Simba inalazimika kuweka nguvu zake zote kweny ligi kuhakikisha inatetea ubingwa wake ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
Kwa sasa Simba haipaswi kupoteza alama zaidi hasa kwa michezo inayopigwa kwenye dimba la Taifa
Ratiba ya michezo ya kufunga mwaka 2018

ADVERTISE HERE