Mwana Msimbazi huwezi kuamini kilichotokea uwanja wa Taifa, kwani yale yaliyotokea msimu uliopita yametokea tena baada Simba kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mashujaa Fc.
Kabla ya mchezo huo mashabiki wengi waliutahadharisha uongozi wa Simba kutowadharau Mashujaa Fc hasa kutokana na kumbukumbu ya msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Green Worriors katika michuano hiyo hiyo.
Licha ya kutangulia kufunga, vijana wa Mashujaa walionekana kuwa wazuri hasa kwenye kipindi cha pili huku wachezaji wa Simba pamoja na mlinda lango Deo Munishi wakifanya makosa mengi ambayo yameigharimu timu kuondoshwa katika raundi ya tatu ya kombe la FA kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Mabao yote ya Simba yalifungwa na Paul Bukaba wakati Mashujaa walijipatia mabao yao kupitia kwa Khamis, Jeremiah na Athumani aliyefunga bao la tatu kwenye dakika za majeruhi.
Simba sasa inalazimika kutetea ubingwa wake ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.