Ishu ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi imeshika kasi ikielezwa Mganda huyo ataondoka Simba siku chache zijazo kujiunga na Kaizer Chiefs baada ya pande zote kufikia makubaliano.
Ili kuhakikisha pengo la Okwi linazibwa mara moja, mshambuliaji wa Nkana Fc Walter Bwalya anatajwa kuwa chaguo la kwanza la kocha Patrick Aussems baada ya kuridhishwa na uwezo alioonyesha kwenye michezo dhidi ya Simba.
Bwalya alifunga bao pekee la Nkana katika mchezo wa juzi ambao Simba ilishinda mabao 3-1.
Baada ya kutinga hatua ya makundi Simba inaruhusiwa uongeza wachezaji kwenye kikosi chake kilichotumwa CAF, ili kukamilisha idadi ya wachezaji 30.
Simba ina nafasi tano za kuongeza kwenye kikosi chake baada ya awali kutuma wachezaji 25.
ADVERTISE HERE