Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho Jumatano wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo wa kombe la FA (ASFC), raundi ya tatu
Simba ambayo juzi ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutolewa na Green Worriors kwenye raundi ya tatu msimu uliopita.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na TFF kuhusu michuano hiyo, michezo yote inatakiwa ikamilike kati ya Disemba 21-26 hivyo Simba na Mtibwa ambazo zilikuwa na michezo ya Kimataifa mwishoni mwa wiki zinatarajiwa kushuka dimbani kesho kukamilisha michezo yao.
ADVERTISE HERE