Simba kutuma mwakilishi Misri

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Dec 2018
Simba kutuma mwakilishi Misri

Uongozi wa klabu ya Simba umesema utatuma mwakilishi nchini Misri kwenye upangaji wa makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Hafla hiyo ambayo itafanyika siku ya Ijumaa, Disemba 28 katika jiji la Alexandrie, itarushwa mbashara runingani.

Rais wa Simba Suedi Nkwabi amesema mwakilishi wa Simba anatarajiwa kuondoka keshokutwa Disemba 27 2018 tayari kwa tukio hilo la historia.

Simba imetinga hatua ya makundi baada ya kuiondosha Nkana Fc kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 baada ya kushinda 3-1 juzi katika dimba la Taifa licha ya kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza.

Nkwabi amesema Simba imedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano hiyo hivyo wataanza maandalizi kabambe baada ya kuwafahamu wapinzani wao katika hatua hiyo.

Kwa sasa Simba inajifua kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi, Disemba 29 2018

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’