Uongozi wa klabu ya Simba umeshitushwa na kifo cha Mwanachama wake Rajabu Kessi aliyefariki jana baada ya kuanguka uwanja wa Taifa wakati akishuhudia mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Simba dhidi ya Nkana FC.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba imesema timu hiyo itashiriki kikamilifu katika shughuli zote za msiba na imetoa pole kwa familia ya marehemu Kessi.

ADVERTISE HERE