Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Simba ilifanikiwa kutinga hatua hiyo jana kwa kuilaza Nkana Fc mabao 3-1 na hivyo kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 4-3 licha ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza.

Simba imeungana na timu nyingine 15 kwenye hatua hiyo sasa ikisubiri kupangwa kwa makundi zoezi ambalo linafanyika jijini Cairo Ijumaa ya wiki hii.

ADVERTISE HERE