Manara awashangaza Wazambia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Dec 2018
Manara awashangaza Wazambia

Ushindi wa mabao 3-1 iliyopata Simba dhidi ya Nkana Fc jana uliwahakikishia mabingwa hao wa Tanzania Bara kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Yalikuwa ni matokeo yaliyopokelewa kwa shangwe na Watanzania wakati huko nchini Zambia huzuni ilitawala baada ya Nkana kuungana na ZESCO kuondoshwa kwenye michuano hiyo.

Lakini jambo lililowashangaza zaidi Wazambia ni idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa jana kuiunga mkono Simba.

Baadhi ya mitandao ya habari za michezo nchini Zambia imeeleza kushangazwa na hali hiyo wakifananisha kuwa mchezo huo ni kama ulikuwa wa timu ya Taifa.

"Wazambia tujifunze kutoka Tanzania. Wenzetu mashabiki wamejaza uwanja wao utadhani inayocheza ni timu ya Taifa"

Lakini wasichojua ni kwamba licha ya mashabiki wa Simba kuipenda timu yao na kuwa nayo bega kwa bega pale wanapohitajika, msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amekuwa akifanya kazi ya ziada kuwahamasisha mashabiki kwenda uwanjani.

Manara anaifahamu vyema kazi yake na ndio maana amekuwa msemaji wa klabu ya Simba kwa zaidi ya miaka mitano.

Msimu uliopita kwenye tuzo za Simba, Manara alishinda tuzo ya kuwa Mhamasishaji bora wa mwaka na hakuna shaka msimu huu atashinda tuzo hiyo pia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’