Simba leo imeungana na timu nyingine 15 kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuilaza Nkana Fc mabao 3-1 ukiwa ni ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Mabingwa hao wa Tanzania sasa wanasubiri kupangwa kwa ratiba ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu 16 zitakazogawanywa katika makundi manne.

Kwa kutinga hatua ya makundi leo Simba imejihakikishia kitita cha Bil 1.2 fedha ambazo zinaweza kuongezeka kama itapenya hatua ya robo fainali, nusu fainali, fainali au kuwa bingwa.
MGAWANYO WA ZAWADI
Makundi - 1.2billion
Robo fainal - 2.1billion
Nusu fainal - 4.0billion
Mshindi wa 2 - 5.0billion
Bingwa - 6.1billion
Droo la hatua ya makundi itafanyika Ijumaa ijayo
ADVERTISE HERE