Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' amewapongeza wachezaji wa timu hiyo na benchi la ufundi kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Simba imetinga makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 bada ya leo kuifumua Nkana Fc mabao 3-1 kwenye mchezo uliopigwa dimba la Taifa.

MO amesema lengo kuu la Simba ni kutwaa ubingwa wa Afrika, hivyo matokeo yaliyopatikana leo ni mwanzo wa kuikamilisha ndoto hiyo.
"Hongereni Simba, Narudia tena: Lengo letu ni kuwa Mabingwa wa Afrika!," ameandika MO kwenye ukurasa wa mtandao wake wa Instagram.
MO ndiye anayechochea mafanikio ya Simba akihakikisha wachezaji wenye sifa wanasajiliwa kutoka mahali popote sambamba na kusimamia maslahi mazuri ya wachezaji hao
ADVERTISE HERE