Vibe kama lote kwa mashabiki wa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Dec 2018
Vibe kama lote kwa mashabiki wa Simba

Wiki iliyopita uongozi wa Simba kupitia kwa Msemaji wake Haji Manara ulianzisha kampeni ya KUFA NA KUPONA kuhakikisha mabingwa hao wa Tanzania Bara leo wanashinda na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa.

Idadi ya kutosha ya mashabiki wamejitokeza uwanja wa Taifa leo na hakika ni furaha kwao kwani wameweza kuandika historia sambamba na kikosi cha Simba kilichotinga hatua ya makundi baada ya ushindi wa mabao 3-1.

Leo ni siku ya furaha kwa mashabiki na kila mmoja aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika mafanikio haya ya Simba yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu.

Benchi la Ufundi na wachezaji wa Simba wanastahili pongezi zaidi kwa kazi kubwa waliyoifanya leo kuhakikisha wanalipaisha jina la Simba na Tanzania barani Afrika.

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji nae anastahili pongezi za pekee kwani uwekezaji wake umeanza kuzaa matunda na hakuna shaka mambo mazuri zaidi yanakuja Msimbazi

Kutinga hatua ya makundi ni mwanzo mzuri kwa kikosi cha Simba katika kampeni yake ya kusaka ubingwa wa Afrika

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’