FT : Simba 3-1 Nkana FC, Chama apeleka kilio Zambia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Dec 2018
FT : Simba 3-1 Nkana FC, Chama apeleka kilio Zambia

Wekundu wa Msimbazi, Simba wametinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa staili ya aina yake baada ya kuifumua Nkana Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa leo.

Bao la kideo lililoipeleka Simba hatua ya makundi liliwekwa kimiani na kiungo fundi, Clatous Chama kwenye dakika ya 88 akimalizia pasi ya Hassani Dilunga 'HD'.

Nkana Fc hawatalisahau bao hilo na hakika Wazambia hao hawatamsahau 'ndugu yao' Chama kwani leo alikuwa kama hawajui.

Ilikuwa ni Nkana Fc iliyotangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Walter Bwalya kwenye dakika ya 17. Bao hilo liliiharibia Simba hesabu kwani awali ilikuwa ikihitaji ushindi wa bao 1-0.

Licha ya kuwa nyuma kwa bao  la mapema, mabingwa hao wa Tanzania Bara hawakukata tamaa na walifanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 30 kupitia kwa shuti la Jonas Mkude aliyemalizia pasi ya Chama.

Meddie Kagere akaiongezea Simba bao la pili kwa kichwa dakika chache kabla ya kwenda mapumziko kabla Chama hajafunga bao la 'usiku' lililoipeleka Simba hatua ya makundi.

Matokeo hayo ni ushindi mwingine wa kihistoria kwa Simba ambayo sasa imerejea hatua ya makundi baada ya kusubiri ka miaka 15.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’