Leo michezo mitatu imepigwa kukamilisha mzunguuko wa 10 ligi kuu ya Vodacom.
Yanga imepata 'vibonde' baada ya kuilaza Mbeya City mabao 5-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru.
Azam FC imeilaza Njombe Mji bao 1-0 huku Mtibwa Sugar ikichapwa kwa mara ya kwanza msimu huu kwa kulala kwa bao 1-0 kutoka kwa ndugu zao Kagera Suagr.
Matokeo hayo hayajaweza kuiondoa Simba kileleni baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Prisons jana.
Simba inaongoza ikiwa na alama 22 ikiwa na tofauti ya mabao (+17) huku Azam FC nayo ikiwa nafasi ya pili ina alama 22 na tofauti ya mabao (+6)
Licha ya ushindi leo Yanga imesalia nafasi ya tatu ikijikusanyia alama 20 na tofauti ya mabao (+12).
Katika orodha ya wafungaji bora bado Emanuel Okwi anaongoza akiwa na mabao yake nane huku Obrey chirwa wa Yanga na Mohammed Rashidi wa Prisons wakiwa na mabao sita kila mmoja.
Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib wana mabao matano kila mmoja.

ADVERTISE HERE