Kocha wa makipa wa kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Mwarami Mohammed amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc utakaopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuelekea mchezo huo, Mwarami amesema wachezaji wamendaliwa kuweza kuibuka na ushindi kesho na kuandika historia nyingine kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Mwarami amewataka mashabiki wote kutoka kila pembe ya jiji la Dar es salaam na mikoa ya jirani kufurika kwa wingi uwanja wa Taifa.
"Tumewaanda wachezaji vizuri tayari kwa mchezo ili tupate ushindi na tuandike historia mpya, ni mchezo muhimu sana kwa klabu. Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi ikiwezakana tuujaze kabisa uwanja," amesema
Simba inahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kufanikiwa kutinga hatua ya makundi. Sapoti kubwa ya mashabiki itaongeza hamasa kwa wachezaji hivyo mashabiki wameaswa kuzima TV zao na kuelekea uwanjani siku ya kesho.