Kiungo wa Simba Mzambia Clatous Chama 'CCC' leo amemzawadia jezi shabiki wa timu hiyo Raphael Oleshang'ai maarufu Mtakatifu Jr.
Kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya Mbabane Swallows uliopigwa uwanja wa Taifa Novemba 28 na Simba kuikuba na ushindi wa mabao 4-1, shabiki huyo aliingia na bango uwanjani akiomba jezi ya Chama.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba mapema leo imesema Chama ametimiza ndoto ya shabiki huyo kwa kumzawadia jezi yake namba 27.
"Mchezaji wetu Clatous Chama amemkabidhi zawadi ya jezi shabiki wa timu yetu, Raphael Oleshang'ai maarufu kama Mtakatifu Jr baada ya siku kadhaa zilizopita picha yake kusambaa katika mitandao ya kijamii akimuomba Chama ampe jezi. Kesho tujitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa tukiwa tumevalia jezi zetu za rangi nyekundu au nyeupe."
Chama aliyetua Simba kutoka klabu ya Dynamos ya Zambia, amekuwa na kiwango kizuri kinachowavutia mashabiki wa soka nchini.