Simba na Mtibwa zina jukumu la kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya vilabu Barani Afrika.
Simba, mabingwa wa Tanzania Bara wanaiwakilisha nchi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakati Mtibwa Sugar mabingwa wa kombe la FA wanaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.
Leo Mtibwa Sugar inachuana na KCCA ya Uganda kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho unaopigwa dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.
Mtibwa Sugar ina mlima mrefu wa kupanda kwani inahitaji kushinda sio chini ya mabao 4-0 ili iweze kutinga hatua inayofuata.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Uganda Mtibwa ilifungwa mabao 3-0.
Walima miwa hao kutoka Turiani mkoani Morogoro wameapa kupindua matokeo leo na kutinga raundi ya pili.
Mchezo mwingine ni wa ligi ya mabingwa ambao utapigwa uwanja wa Taifa kesho Jumapili kati ya Simba dhidi ya Nkana FC.
Simba itahitaji kushinda bao 1-0 ili kutinga hatua ya makundi.
Kila la kheri wawakilishi wa nchi.