Klabu ya AFC Leopards inayoshiriki ligi kuu ya Kenya imemtambulisha mshambuliaji Marcel Kaheza aliyetua timu hiyo kwa mkopo wa miezi sita akitokea klabu ya Simba, mabingwa wa soka Tanzania Bara.
Kaheza ameungana kucheza ligi kuu ya Kenya na beki wa zamani wa Simba Jamal Mwambeleko ambaye alisajiliwa na KCB.

Tunawatakia kila la kheri wachezaji wote waliotolewa kwa mkopo naamini watafanya vizuri huko walikoenda na kurejea wakiwa imara kuwania namba latika kikosi cha kwanza cha kocha Patrick Aussems.
ADVERTISE HERE